Hawa ni wachezaji ambao wameongeza mikataba yao kwenye timu ya Kagera Sugar kwa miaka miwili zaidi katika dirisha hili la uhamisho.

Wachezaji hao ni Ally Nassoro, Apolinaire Ngueko, Said Kipao, Abdallah Seseme, Mbaraka Abeid na Ramadhan Chalamanda.

Pia wamesajili kiungo wa kati Datius Peter kutoka timu ya Polisi Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili.

Mchezaji huyo alitambulishwa rasmi kwenye kikosi hicho mnamo Jumanne, Julai 19.